Utalii
Tasnia ya utalii ya Tanzania ina uwezo mkubwa sana wa kuendelezwa. Kuna vivutio vya asili kama vile mandhari za kuvutia, maeneo ya kihistoria na ya kiakiolojia, hifadhi zenye wanyama wengi, fukwe zisizochafuliwa na wingi wa utamaduni wa makabila 158. Nyanda za juu za kusini na kaskazini zina safu nyingi za milima ya kuvutia hasa yenye urefu wa kati ya mita 500 mpaka mita 1000 kuliko maeneo yaliyoizunguka. Milima ya Kilimanjaro na Meru iliyopo kaskazini mashariki ni volkano za kale, yenye urefu wa mita 5,895 na 4,500 kwa mfuatano huo. Mwambao wa bahari una urefu wa zaidi ya kilomita 804 pamoja na visiwa vya jirani vya Unguja (kinachojulikana kuwa Zanzibar), Pemba na Mafia. Visiwa hivyo vina mkusanyiko wa vivutio vya asili, utamaduni, historia na akiolojia. Maliasili nyingine ni pamoja na Ziwa Viktoria, ziwa la pili kwa ukubwa duniani, na chanzo cha mto Nile.
Subscribe to:
Posts (Atom)
0 comments:
Post a Comment