Afya Na Mazingira

Sehemu hii ya Chakula, Maji, Usafi na Afya Mazingira inafanyakazi kuhakikisha upataji endelevu wa afya mazingira bora, hali bora ya afya na usafi kwa jamii za mijini na vijijini, ili kufikia lengo la kuwa jamii yenye afya na maisha bora itakayochangia kwa ukamilifu maendeleo ya mtu mmoja mmoja nay a taifa.
Afya mazingira ina athari kubwa ya pili ya kupunguza kuharisha na kupunguza athari kwa kiasi cha asilimia 36. Uhakika wa chakula, upataji wa maji safi na salama ya kunywa na vyoo bora vinavyoweza kusafishwa wakati wote na  kunawa mikono kwa sabuni kuna matokeo makubwa katika kupunguza uambukizaji wa magonjwa, ikiwemo kuharisha, kupunguza  hali hiyo kwa asilimia 47. Hata hivyo elimu kuhusu umuhimu wa tabia za usafi, hasa kunawa mikono kwa sabuni, ni za kiwango kidogo. Sehemu hii inahakikisha kwamba watu wanapata chakula chenye lishe/virutubisho vya kutosha na maji salama ni muhimu kwa kulinda usalama, afya na ustawi wa kila mmoja, hasa kina mama wajawazito na watoto.
Si maji ambayo ni muhimu tu kuendesha maisha, lakini lishe bora nayo inatakiwa, aina mbalimbali za chakula , zenye vitamin na madini ya kutosha, ni msingi wa mlo wenye afya. Watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wako hatarini zaidi kupata utapiamlo. Ili kuepuka ukosefu wa lishe unaosababisha uchovu na udhaifu, unakwaza au huduma za ukuaji wa mwili na akili, hasa kwa watoto (ambapo husababisha kudumaa) na kuongeza urahisi wa kuambukizwa magonjwa mengine ya hatari kama vile kichomi na kuharisha, hatua  zinachukuliwa kuboresha chakula, Maji, Usafi na Afya mazingira nchini.
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2013-07-24 08:37:43

0 comments:

Post a Comment