Mambo kadhaa yanayoweza kukufanya kuwa mbunifu:-

1Ondoa uwoga: Usiogope kuwa wazo lako litakuja kushindwa. Chukulia kuwa hata kama litakuja kushindwa, utakuwa tayari umeshapata uzoefu wa kutengeneza wazo lingine bora zaidi.

2. Usijilinganishe na watu wengine:  Usiangalie wengine unao dhani wamekuzidi uzoefu au ujuzi wamefanya nini , kiasi kwamba ukajishusha kuwa eti wewe hauwezi kufikia kuwa na kitu kizuri cha ubunifu.

3. Zingatia Upekee: Kama unataka kufanya UBUNIFU , lakini mawazoni mwako unapata ukinzani wa kutaka kufanya kama fulani, basi ujue hapo kuna tatizo. Sisitiza kuwa na upekee, na upekee tuu ndio utakaoleta maana haswa katika ubunifu wako, hata mbele za wateja. Hata hivyo hii haimaanishi kuwa hautakiwi kuangalia wengine wamefanya nini, hapana, angalia wengine kwa lengo la kujifunza, na kutambua mapungufu.

4. Zingatia kukidhi mahitaji ya binadamu:  Ubunifu wako hautokuwa na maana kama haukidhi mahitaji ya watu. Hivyo njia rahisi ya kuanza ubunifu ni kuisoma jamii, kuangalia matatizo yanayoikumba jamii. Sio lazima uangalie mbali sana, waweza hata kutafakari matatizo ambayo yamekuwa yakikutatiza wewe mwenyewe, kisha ukaamua kubuni kitu cha kuleta suluhisho. Fanya uchunguzi kujua wengine wamekumbana na matatizo kama yako.
Mfano mzuri,Drew Houston mwanzilishi wa huduma ya kuhifadhi documents online,  DROPBOX anasema alianzisha huduma hiyo baada ya yeye mwenyewe kuwa mpotezaji wa flashdisk wakati akiwa chuoni MIT.

1 comments:

  1. habari zenu wasomaji wa blog hii? karibuni tena kwa masomo mbali mbali, ushauri na maoni yenu tafadhali ni muhimu sana kwetu.

    ReplyDelete